Jumapili, 2 Oktoba 2016

NA.41 - NA.45: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.



  • Siri ambazo nimekuwa nikizichambua na kuziainisha hapa miongoni mwetu wengine wanawaza mafanikio ya pesa tuu. Naomba kadiri tunavyoendelea tutafakari zaidi ya hapo. Kiongozi ukisimama vizuri kwenye nafasi yako ni mafanikio; ukijua ulipo, unakoelekea ni mafanikio pia; ukijitambua ikiwa akili yako iko sawa ni mafanikio pia; kudumisha amani katika ndoa au familia ni mafanikio pia; ukijua mahitaji ya unaowaongoza na ukayatatua ni mafanikio pia; matatizo makubwa yanayotufanya tusifikie ndoto zetu ni mtu mwenyewe siyo pesa, pesa inakuja kulingana na wewe mwenyewe ulivyojiweka. Tuendelee sasa kuangalia mfululizo wetu:-

  1. Ukisimama na kuongea na mtu, simama sawasawa na kiumadhubuti. Ishara zinazoonesha kutokuwa makini, uwezo mdogo ni kutokutulia, kupepesapepesa macho na upumuaji usio makini pamoja na vyote kama hivyo jitahidi kuvidhibiti.
  2. Onyesha uhodari na utakuwa hodari. Jipe moyo na utafanya wengine wakupende kwa vitendo vyako. Na wakati wote fanya kwa busara.
  3. Usiulize dunia itakufanyia nini, bali jiulize utafanya nini kwaajili ya dunia. Huduma zako zifanye kitu cha msingi katika maisha yako. Ni uwekezaji wa muda unaojitosheleza. Kumbuka, utusiutusi wa maisha yako, wengine wote wanapokuwa wamesema na imekuwa, ubora wa maisha yako unapoa kutokana na mchango wa ubora wako kwa wengine waachie waliokuzunguka ladha na harufu ya uhalali wa utajiri wako.
  4. Mara moja katika wiki inuka wakati wa mawio. Ni siku ya muujiza kwako. Tulia, nenda matembezi, oga maji ya manyunyu ya uvuguvugu na fanya mazoezi ya “push up” kama 100. Soma moja ya maandiko bora kabisa. Utajisikia mwenye afya nzuri na utajipa moyo sana.
  5. Baki katika hali ya kujitenga kidogo. Usifanye kila mtu afahamu chochote kuhusu wewe. Jenga hali ya kuwa na ustadi wa peke yake.
Kwa leo naishia hapa,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843 804
Endelea kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com

Hakuna maoni: