Jumamosi, 1 Oktoba 2016

NA.33 - NA.40: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA



  1. Nyakati hizi tunazoishi maarifa yameongezeka sana! Ni kwa msingi huo utaona vitabu vingi sana vinatolewa kwa njia ya sauti ambapo badala ya kusoma unasikiliza tuu. Ni vizuri kusikiliza maarifa hayo ya kuvutia ambayo yanajenga na kuupanua uelewa wako na hivyo kufanya huduma zako kuongezeka thamani siku baada ya siku kutokana na kusikiliza maarifa hayo na kuyafanyia kazi. Fanya mazingira ya gari yako kuwa chuo cha maarifa, ofisini kwako na popote unapopata muda wa ziada katika kusikiliza na kufuatilia maarifa hayo ndivyo utakavyo fanikiwa katika maisha yako.
  2. Jaribu kuwa na kipindi cha kufunga walao mara moja kila wiki mbili. Wakati huo wa kufunga kunywa angalao juisi ya matunda na vyakula laini na vipya yaani “fresh food” tuu. Kwa kufanya hivyo utajisikia mwili unaongezeka nguvu na zaidi wepesi katika mwili. Kufunga huuburudisha mwili na kuongeza uwezo wa kutafakari.
  3. Unapokuwa ofisini au katika kazi ambazo zinahitaji utulivu ili kuongeza ari na kuipenda zaidi kazi yako fungua muziki laini katika komputa yako ambao huondoa ukimya na kuongeza moyo wa kuyapenda sana mazingira yako na kazi yako unayoifanya. Aidha ni vizuri kuwa na ratiba walao ya dakika 30 kutembelea maktaba za vitabu ambako unaweza kukutana na vitabu au tepu za kurekodi sauti ambazo ni matoleo mapya yenye maarifa mbalimbali.
  4. Soma kitabu kiitwacho “As a man Thinketh” kama kilivyoandikwa na James Allen. Na usisome kitabu hiki mara moja tuu bali rudia tena na tena. Kitabu hiki kina wingi wa hekima na maarifa ambayo yanaweza kukufanya uishi maisha yaliyojaa furaha.
  5. Kumbuka msamaha ni hazina kubwa sana ambayo ni wachache wanayo, kitu kimoja cha msingi ni kutunza amani ya akili yako. Mark Twain aliandika kwamba “msamaha ni kama manukato ambayo hufunika harufu mbaya” Jaribu kusamehe zaidi kwenye mazingira yanayoonekana kuwa magumu. Kuonyesha hali ya kusamehe inakujengea umakini zaidi katika kutafakari na inakupunguzia makosa madogo madogo katika utendaji wako na hakuna chochote kitaharibu jambo unalolitafakari.
  6. Kifanye kikombe chako kuwa kitupu. Kikombe kilichojaa hakiwezi kupokea kitu kingine zaidi hii ni sawa mtu anaye amini kuwa hawezi kujifunza au kusoma zaidi, atadumaa na kamwe hawezi kupiga hatua nyingine yeyote bali atabaki hapohapo. Alama kuu ya ukomavu na kujiamini kwa mtu ni jinsi kila fursa inayoonekana au kutokea mbele yako unavyoiona kuwa ni nafasi adimu iliyokuja mbele yako ili ujifunze. Kumbuka, “hata walimu wana walimu”.
  7. Dakika mbili za kufikiri ni zoezi zuri la kukuza kutafakari kwako. Fikiri kama ungetumia dakika mbili kukaa bure bila kufikiri chochote. Kwa mara ya kwanza utajishangaa lakini baada ya siku 21 za mazoezi haya ya kutafakari umakini wako hauwezi kutoweka. Kitu kimoja cha thamani ambacho binadamu yeyote anapaswa kukijenga ndani mwake ni uwezo wa kuwa na maono ya mbali kwa muda fulani. Jenga msuli wa kutafakari na hakika hakutakuwa na kitu chochote kigumu mbele yako.
  8. Kunywa maji ya uvuguvugu kabla ya kunena mbele ya hadhira yako. Ronald Reagan aliitumia mbinu hii kuhakikisha sauti yake nzuri haibadiliki. Ukiweza kutawala namna ya kunena mbele ya hadhira una tuzo kuu. Eneo hili si la kufanyia mchezo. Watu watakuelewa wewe ni nani kwa uwezo ulionao katika kuongea mbele yao

Kwa leo naishia hapa,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843 804
Endelea kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com

Hakuna maoni: