- Msongo wa mawazo ni matokeo ya namna jinsi unavyotafakari jambo au tukio fulani. Ni muhimu kufahamu binadamu hutofautiana na namna jinsi tunavyochukulia jambo lolote tunaloliona kwa pamoja. Mfano mtu mwingine akiambiwa baada ya chakula cha jioni utatoa nasaa kidogo katika kusanyiko tutakalo kuwa nalo atashtuka sana na kufadhaika moyoni ingawa mwingine ataiona ni fursa ya ajabu na atafurahia sana. Fahamu kwamba jambo lolote unalolidhania kuwa na matokeo hafifu waweza kuliangalia kwa upande mwingine na kuona kuwa na matokeo mazuri nay a kutia moyo, huu ni mtizamo tuu unaoweza kukufanya uwe ni mtendaji mashuhuri katika malengo yako.
- Soma “tabia 7 za watu waliofanikiwa” kama ilivyoandaliwa na Stephen Covey (https://www.stephencovey.com/7habits/7habits.php). Hapa kuna utajiri mkubwa wa hekima na utambuzi wenye kukupa nguvu katika kukujenga kitabia na kuimarisha kujiamini kwako.
Kwa
leo naishia hapa,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843
804
Endelea
kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni