Mpendwa msomaji salaam! Leo tuendelee kuangalia siri ambazo bila shaka zaweza kuwa ni kichocheo kikubwa kwa kufikia ndoto ya mafanikio yako;-
- Ukweli, ustahilivu, uvumilivu, kutojivuna na ukarimu ni tabia ambayo kila unayetaka kufanikiwa katika maisha unapaswa kuwa nayo na kama hauna basi jitahidi kuwa hivyo.
- Baada ya shughuli zako za siku ni vizuri ukapata maji ya uvuguvugu kwaajili ya bafu. Jipe moyo na kujipongeza mwenyewe japo kwa mafanikio kidogo yaliyoonekana katika siku yako. Kwa lengo la kuipumzisha akili yako, mwili na roho yako ni vizuri ukatoka na kutembea kidogo nje ya mazingira uliyozoea. Utashangaa baada ya siku chache unayafikia malengo yako ya kipaumbele na kukufanya uendee hatua nyingine.
- Jifunze nguvu iliyopo katika kupumua na mahusiano ya nguvu zako. Kuna mahusiano makubwa kati ya upumuaji na ufahamu wako.Mfano pale ambapo una kufadhaika utaona na upumuaji wako unabadilika na kuwa wa haraka na kuyumba yumba. Ukitulia upumuaji wako huwa wa utulivu na wa chini. Ukijizoesha kupumua vizuri hata utakapokutana na mazingira ya kukustua bado utajiweka katika hali ya utulivu na ustahilivu. Kumbuka kanuni ya Watu wa Milima ya Mashariki “ kupumua sawa sawa ni kuishi sawasawa”.
- Maneno yatokayo katika vinywa vyetu yana nguvu ya kushawishi ufahamu wetu. Ukisema maisha ni magumu ndivyo itakavyo kuwa, au ukijiambia mimi siwezi kufanikiwa ndivyo inavyokuwa pia. Hivyo basi ni vyema kujipa moyo hata pale matokeo yanapokuwa hafifu kinyume na matarajio. Ni vizuri kuwa na tabia ya mwanariadha ambaye kadiri anavyokaribia kilele cha mbio zake, mashindano katika akili yake huwa ni makubwa sana, lakini kwavile amedhamiria kufika mwisho huangalia lengo lake la kufika mwisho hata kama anaoshindana nao watamtangulia sana.
- Kupima mafanikio kwa kuandika katika notebook yako ni jambo lisiloepukika ikiwa unakusudia kufanikiwa katika maisha. Andika mafanikio, andika changamoto unazokutana na angalia namna ya kuzikabili changamoto hizo ili kesho ufanye vizuri zaidi.
Kwa
leo naishia hapa,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843
804
Endelea
kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni