Jumatano, 28 Septemba 2016

NA.21 - NA.25: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.

Mpendwa msomaji wa ujasiriamaliafya, leo tuendelee kuangalia baadhi ya siri za mafanikio katika maisha na hapa nakuletea siri ya 21 hadi 25, hebu fuatana nami;


  1. Hakuna mtu anayeweza kukufedhehesha au kukusononesha bila wewe mwenyewe kuufungua mlango. Ufunguo mkuu wa furaha na mafanikio yako ni namna unavyotafsiri mambo mbalimbali yanayojitokeza mbele yako. Watu mashuhuri waliofanikiwa katika maisha yao ni wale wenye uwezo mkubwa kutafsiri kila jambo analokutana nalo mbele yake. Akikutana na changamoto yeye anazigeuza changamoto kuwa ni fursa yake ya kumfanya aende mbele zaidi. Hakuna jambo lolote analolihesabu kuwa ni kikwazo cha kumfanya ashindwe bali yote anayachukulia kama masomo kwake.
  2. Fanya mazoezi ya kusoma kwa kasi. Kusoma ni namna yakukufanya upate uzoefu wa kutenda mambo mengi zaidi katika maisha yako yote kutokana na masaa machache tu ya kusoma. Kusoma kwa kasi kunakufanya upate maarifa mengi sana kwa muda mfupi sana.
  3. Jitahidi kuyakumbuka majina ya watu unaokutana nao katika biashara zako uwathamini na kila mmoja mhudumie kulingana na alivyo.  Tabia hii sambamba na shauku ni siri kubwa sana ya mafanikio. Watu wengi hupenda kutambuliwa kuwa ni wa muhimu na kuheshimiwa.
  4. Inapokuja hali ya upole jiweke katika hali ya mvuto kama Ua na katika kusimamia misingi yako unapaswa kuwa thabiti kama radi. Uwe na heshima na adabu, lakini kamwe usiyumbishwe. Jenga mazingira ambayo yeyote atakustahi.
  5.  Kamwe usijadili kuhusu afya yako, utajiri wako au lolote la binafsi na yeyote nje ya familia yako. Eneo hili unapaswa kuwa makini sana.
Kwa leo naishia hapa,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843 804
Endelea kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com

Hakuna maoni: