- Kwanini usitumie muda na uwezo ulionao kujikita katika eneo Fulani litakalo kupa umaarufu na kukujengea uzoefu kwa muda mfupi hata uishangaze dunia!? Fahamu kuwa muda wetu hapa duniani ni mfupi sana! Sasa je unashindwa kujitoa kwaajili ya jambo linaloweza kukufanikisha na kukupa furaha kwa kipindi hiki kifupi!? Hebu keti chini na uorodheshe yote uliyonayo mpaka sasa. Anza na suala la afya yako na familia yako kama mambo yanayotupa kibali cha kuendelea na mambo mengine. Andika kuhusiana na nchi yako unayoishi na chakula unachopenda kutumia kila siku. Usiache mpaka walao umefikisha mambo 50. Baada ya hapo kila baada ya siku kadhaa pitia orodha hiyo na utatambua utajiri mkubwa ulio nao ambao umekuzunguka, hali hii itakuhamasisha na kukupa hasira zaidi ya kuuchukia umasikini na utagundua ni ridhaa yako tuu ndiyo inahitajika.
- Ni lazima uwe na dira ya kukuongoza katika maisha yako. Hili litakusaidia kujitambua upo wapi na mwisho wa siku au uhai wako duniani unataka uweje na unaendeleaje!? Siku zote dira hupamba thamani ya maono yako. Dira yako inakuongoza na kukufanya uendelee kusimamia ndoto zako pia. Ni muhimu pia kuketi chini na kuandika misingi mitano au kumi unayoamini inaweza kukufanya kusimamia dira yako na kukufanya usiyumbishwe na lolote. Hapa itakusaidia kutoyumbishwa na chochote, inawezekana umeamua uwe mtumishi wa watu, au uwe kiongozi bora, au uisadie jamii. Pale utakapogundua umeyumbishwa na lolote iwe ni changamoto ulizokutana nazo au lolote itakufanya urudi haraka katika yale unayoyasimamia.
Kwa
leo naishia hapa,
\\ujasiliamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843
804
Endelea
kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiliamaliafya.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni