Jumatatu, 26 Septemba 2016

NA.16 - NA.18: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA



  1. Ifanye siku nzima kuwa ni siku ya kufurahi na kuchangamka kwako. Hii itakusadia si wewe tu lakini hata mazingira mbalimbali tatanishi unayokutana nayo utatanishi huo huondolewa na tabia yako ya ucheshi. Yapo makabila mbalimbali ambayo hata usiku wa manane huamka na kwenda kumfanyia jirani yake jambo litakalo mfanya afurahi. Mfano kule Amerika ya Kusini ililipotiwa kuwa ipo jamii moja ya watu waitwao “Tauripan” hawa huamka hata katikati ya usiku na kwenda kumchekesha tuu mwenzake.
  2. Nidhamu katika kuutawala muda. Katika wiki moja kuna wa masaa 168 ambayo kama mtu umekusudia kuyatumia vizuri, mambo mengi sana unaweza kufanya. Uwe katili katika kuutumia muda wako usiuonee huruma. Asubuhi unapoamka tenga dakika chache kupangilia yale unayokusudia kuyafanya kwa siku nzima. Unapopangilia yale ya kuyafanya kwa siku nzima hunabudi kutanguliza yale yaliyo kipaumbele katika mipango yako na ni muhimu kutekelezwa katika siku yako. Kuna weza kuwa na jambo ambalo ni la muhimu lakini si lazima kulifanya sasa. Vitu vya muhimu lakini si lazima kwa sasa ni vile vyote vinavyoleta matokeo baada ya muda mrefu. Mfano; mazoezi, mpango mkakati na au mahusiano katika maendeleo yako. Kamwe usikubali mambo ya msingi uliyokusudia kutekeleza katika siku husika muda wake kuchukuliwa na vitu vingine.
  3. Kubali kuambatana na watu ambao wana mtizamo chanya na kamwe usikubali kuambatana na watu walalamishi na wepesi kukata tama kwani kuambatana na watu wa jinsi hii wataondoa hata kile kizuri kilichopo ndani mwako. Kwa kuwa na mahusiano na watu walao wenye mtizamo wa kati itakusaidia kujifunza mengi na itakuwa ni chachu ya ari kwako katika kuyafikia mafanikio yako. Na hapa utaona hata kama ulitaka kulifanya jambo kubwa kiasi gani utafikia bila shaka!.

Hakuna maoni: