Jumapili, 25 Septemba 2016

PEPTIC ULCERS AU VIDONDA TUMBO: MSAADA MBALI NA DAKTARI.


Kuna magonjwa ya matumbo yajulikanayo kitaalam kama Peptic Ulcer (Gastric Ulcer, Stomach Ulcer, Duodenal Ulcer) au kwa lugha iliyozoeleka kama Vidonda vya tumbo.
Magonjwa haya yote kwavile yote ni ya tumboni wapo watu wengi wameteseka nyakati ambazo Daktari hayupo au wapo mbali na matabibu na hata kupoteza maisha. Mimi ndugu yako leo naomba tusaidiane ni namna gani utakabili hali hii pasipo daktari. 
DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA TUMBO. 
·         Maumivu makali yenye dalili za kiungulia dakika 45 - 60 baada ya kula chakula au wakati wa usiku. Ukinywa maji glasi moja kubwa au ukila chakula utaona kuna kutulia. Wakati mwingine kutapika na kukudhohofisha mwili. Wakati mwingine yataanza majira ya saa saba hadi saa nane usiku. Maumivu chini ya kifua yanayoendelea. Hii ni dalili ya vidonda vya tumbo bila ubishi.Maumivu haya wakati mwingi wengi husema ni kiungulia au njaa.
·         Dalili zingine ni kama; Maumivu ya kichwa,kuhisi harufu mbaya, Maumivu chini ya mgongo, Kuwashwa na au kutapika.
SABABU:
·         Sababu ya magonjwa haya wataalam wanatuambia ni ulaji chakula usio stahili au ulaji chakula unaopita kipimo. Wakati mwingine inakuwa ni sababu ya msongo wa mawazo au maumivu ya neva katika miili yetu.
·         Kuta za matumbo yetu huzalisha asidi iitwayo inayofanya kazi ya kuyeyesha protein mwilini mwetu. Licha kuwa kuta zenyewe za matumbo yetu yenyewe yana proteini, asidi hiyo hainaga madhara kwenye matumbo yetu ingawa chakula tunachokula au matatizo ya hali ya mtu ndipo shida huanza. Matatizo hayo hupelekea aside hiyo kuyeyusha kuta za matumbo yetu kwasababu asidi iliyozalishwa imezidi au ute unaolinda kuta hizo unapokuwa hauzalishwi vilivyo.
·         Vidonda hivi vya tumbo hutokea kwenye esophagus au umio, lakini kawaida hutokea kwenye tumbo au utumbo mwembamba. Vidonda vya tumbo hutokea mara 2 ½ zaidi kwa wanaume zaidi ukilinganisha na wanawake kwenye umri wa miaka 40-55. Vidonda vya tumbo katika utumbo mwembamba hutokea kwa mara ya kwanza inchi 11 tokea tumboni yaani stomach nah ii ni kwasababu ya kuzidi hiyo asidi iitwayo HCL. Vidonda tumbo hivi hutokea zaidi kwa wanaume mara nne zaidi ya wanawake kwenye umri wa miaka 25-40.
·         Huko Amerika 15% ya watu wake wana vidonda tumbo. Lakini ni nusu yake tuu ndio hutibiwa. Wengi hugundulika baada ya kuanza kutapika damu. Vitu vinavyochangia kuzalishwa kwa hiyo asidi HCL mwilini zaidi ya kawaida ni pamoja na wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo. Aspirini, dawa za kuzuia uvimbe na uvutaji sigara vyote hivi vinaongeza HCL kwenye matumbo.
·         Unaposikia maumivu ya tumbo kwa dalili nilizoorodhesha hapo juu kunywa juisi ya limao ukiona hali inazidi basi fahamu HCL imezidi kwenye matumbo. Na kama unatapika damu au unapata choo chenye damu una hatari ya kuvuja damu hadi kifo unapaswa kuwahi kuwaona matabibu Hospitalini. Na kama ukinywa juisi ya limao na maumivu yakatoweka basi fahamu una upungufu wa HCL kwenye matumbo yako.
MATIBABU PASIPO DAKTARI:
·         Kunywa maji katika glasi kubwa ili kuondosha maumivu kwa haraka.
·         Maji yanapunguza nguvu ya asidi na kutoa nje asidi hiyo.
CHAKULA:
·         Kula chakula kidogo siyo mpaka uhisi tumbo limejaa.
·         Viazi mviringo ni vizuri zaidi.
·         Juisi ya kabichi ukichanganya na karoti na uinywe mara 4 kwa siku.
·         Kula mbogamboga kwa wingi.
·         Mchele mweupe na mtama uliopikwa vizuri pia unafaa.
·         Maziwa pia si mazuri kwa mgonjwa wa vidonda tumbo maana yanafanya asidi izalishwe zaidi.
·         Madaktari wa india wanatumia unga wa ndizi kutibu vidonda tumbo hivyo basi ndizi mbivu ni nzuri pia.
·         Kula vyakula vingine vyenye vitamin A, Zinc, Copper, Glutamine kadiri matabibu watakavyokushauri.
EPUKA:
·         Epuka mazingira yote yanayokufanya uwe na wasiwasi, msongo wa mawazo, na au uoga.
·         Epuka vyakula vilivyo na caffeine, uvutaji sigara, na usinywe maziwa ya ng`ombe.
·         Matumizi ya chumvi yaliyozidi.
·         Chakula chenye sukari nyingi.
·         Mkate mweupe yaani white bread.
·         Kula bila utaratibu.
·         Dawa za kutuliza maumivu.
MAMBO MENGINE YA KUFANYA:
·         Mazoezi ya wastani hupunguza msongo wa mawazo.

Hakuna maoni: