Jumapili, 25 Septemba 2016

NA.11 - NA.15 MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA



Mpendwa msomaji wa Makala za www.ujasiriamaliafya.blogspot.com Leo tuendelee na mfululizo wa siri za mafanikio katika maisha, na hapa tutaangalia mfululizo Na. 11 hadi Na. 15.
Fuatana nami sasa;
  1. Washa mshumaa pembeni yako wakati unasoma vitabu mbalimbali au makala mbali mbali zinazozidi kukupa hamasa katika kuyaendea yale uliyokusudia mbele yako huku ukisikiliza muziki wa ala laini unaofanya eneo liwe tulivu, hili litakufanya ufurahie eneo la nyumbani kwako mbali na dunia hii yenye masumbufu mbalimbali. Tafuta makala maarufu na bila shaka hata ukijipatia marafiki maarufu watafurahia kukaa hapo nyumbani na wewe na kuondoa kabisa upweke.
  2. Wakati unatembea kwa mguu jaribu kuhesabu hatua zako, hii ni mbinu inayokujenga kuwa mtu wa kutafakari na kufikia malengo katika mipango yako. Jaribu tena kwenda hatua sita bila kuvuta pumzi na rudia tena hatua sita huku unatoa pumzi. Ukifanya hivyo utajisikia vizuri sana maana watu wengi huruhusu akili yao kujaza na kutafakari vitu ambavyo hatimaye huwa ni chanzo cha maradhi mbalimbali ya mwili. Jifunze kupunguza msongo akilini kwa mbinu kama hiyo. Aidha ikumbukwe kwamba watu waliofanikiwa sana wanatambua nguvu ya utulivu, akili isiyo na msongo wa mambo yasiyo na tija na kuutumia ubongo kufikiri zaidi juu ya mambo ya msingi na yenye tija.
  3. Jifunze namna ya kutafakari sawasawa. Kwa asili ubongo wa mwanadamu ni kama mashine inayokimbia sana. Hutaka utoke kwenye jambo moja na uende kwenye jambo lingine haraka sana usipodhibitiwa. Kutafakari kwa dakika 20 asubuhi na dakika 20 jioni kwa muda wa miezi sita mfululizo kwaweza kukuletea mabadiliko na ushindi mkubwa sana katika kuelekea mafanikio ya kweli katika maisha yako. Wenye hekima na waliofanikiwa kwa wingi mashariki ya mbali wamekuwa wakitumia nguvu ya kutafakari katika ubunifu wa mambo mbalimbali kwa takribani miaka 5000 iliyopita. Na wengi wetu ni mashahidi.
  4. Jifunze kutulia. Watu wengi hawawezi kutulia kwa dakika angalau 30 ndani ya mwezi mzima kwa ukimya na utulivu. Jikuze katika kuketi na kutulia kwa utulivu na ukimya walau dakika 10 kwa siku. Hii inakurahisishia kufikiri ni kipi cha muhimu kwa maisha yako. Katika utulivu huo akisi yale unayotaka kuyafikia. Utulivu ni kitu cha thamani kubwa sana.
  5. Ongeza nguvu ya ridhaa yako; ukifanya vizuri hapa unakuwa umewekeza kama kwenye programu ya mafunzo ya muhimu sana kwako; hapa sasa tuangalie dhana mbalimbali katika kuongeza nguvu ya ridhaa yako;
a)    Usiache mawazo yako mazuri kuelea juu kama karatasi linalopeperushwa na upepo, endelea kujitahidi katika kuelekea malengo yako ya mafanikio. Unapofanya jambo moja usiruhusu akili yako kuwaza jambo lingine. Kama unatembea kwenda kazini kwako hesabu hatua zako ili kuufanya ubongo wako kutulia na jambo moja. Hapa siyo kazi rahisi lakini kadiri unavyojizoeza basi akili yako itafahamu mbele nini ulikuwa unafanya.
b)    Ridhaa yako ni kama misuli. Kabla misuli haijawa imara inategemea bidii ya mazoezi yako. Muhimu kufahamu maumivu yanakuwa unapoanza lakini kadiri unavyoendelea kujizoeza basi mafanikio utayaona mbele yako. Mfano kama una njaa kali sana basi ongeza saa moja mbele ndipo utafute chakula. Sir Issac Newton Mwana fizikia maarufu alisema “ ikiwa nimefanya jambo lolote zuri mbele ya jamii basi ni baada ya kupitia maumivu katika fikra” Newton huyu anakumbukwa kwa uwezo wake usio wa kawaida wa kukaa muda mrefu katika utulivu mwingi bila kuingiliwa na chochote. Ikiwa yeye aliweza akipitia njia hiyo wewe na mimi twaweza bila shaka!
c)    Unaweza kujenga nguvu ya ridhaa yako kwa kujitenga na wengine. Ongea maneno machache kwa kanuni ya 60/40 (yaani unapokea maneno 60% na unajibu au unaongea maneno 40%), tabia hii haitakufanya uwe maarufu tu bali itakufanya uonekane mwenye hekima, kwani katika siku tunakutana na mambo mengi sana na tunajifunza mengi sana katika yale tunayokutana nayo vipo vitu vingi vya kujifunza. Na pia jiepushe kumlaumu yeyote unayedhani amekosea au kumteta. Jitahidi sana kujiepusha na tabia ya kulalamika bali jenga maisha yenye furaha na kujiamini ndivyo utakavyowashawishi na kuwafanya wengi wavutiwe na tabia yako.
d)    Jitahidi kila mawazo hasi na mtizamo hasi unapokuja mara moja tafuta wazo chanya na ndivyo utakavyojiweka katika hali nzuri zaidi. Kwani mawazo chanya siku zote hufuta mawazo hasi. Ni suala la kujipa moyo kwamba hata kama mazingira yanaonekana ni magumu kiasi gani jipe moyo kwamba yana muda tu lazima ufike kwenye malengo yako ya mafanikio. Ni wajibu wako kujikinga na mawazo hasi kwani huja mara kwa mara lakini wewe jiweke katika hali ya kuwa mtu wa mtizamo chanya wakati wote.

Kwa leo naishia hapa,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843 804
Endelea kufuatilia zaidi kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com

Hakuna maoni: