. 117.Katika maswali yote tunayojiuliza siku zote ni muhimu kufahamu hakuna swali
lililo jipya na majibu yake yote yapo tayari! Ni jinsi gani ya kuboresha
uzungumzaji mbele ya jamii, jinsi gani ya kudumisha mahusiano na wengine, jinsi
gani ya kukuza kumbukumbu – vitu vyote vya maendeleo binafsi vinapatikana
vitabuni. Sasa basi ili ufanikiwe katika yote ni wajibu wako kusoma kila siku.
Lakini katika ulimwengu wa sasa wa habari ni lazima usiwe na huruma juu ya nini
unatumia. Lenga mwisho wake na soma vitu ambavyo unadhani ni rasilimali kwako
mwisho wa siku. Usitake kusoma kila kitu huku ukizingatia unayo majukumu
mengine ya kutekeleza, soma vile vya muhimu na achana na vile unavyodhani si
vya muhimu kwasasa. Anza kusoma habari zilizo ngumu asubuhi ili mwisho wa siku
uwe na muhtasari mzuri kwa siku nzima. Katika kusoma hakikisha unajiongeza
ukilinganisha na mazingira yako. Mfano unataka kusoma mambo ya historia
mbalimbali, biashara au falsafa za watu mbalimbali mashuhuri, habari za afya,
n.k. tembelea maktaba na kujijengea mazoea ya kufanya hivyo mara kwa mara. Soma
historia na mafunzo yake yote, soma bailojia kwa mtizamo mpya. Angalia vitabu
au makala zenye kichwa “mafanikio” na utashangaa habari na mambo utakayo
yapata: habari za kuvutia toka kwa watu mashuhuri waliofanikiwa kutoka katika
mazingira yasiyoelezeka, mbinu mbalimbali za kujiimarisha wewe mwenyewe
binafsi, kiakili na kiroho, na makala za kukuunganisha kwenye nguvu za
mafanikio ambazo zipo katikati yetu. Jizamishe sana katika vitabu hivyo.
Jijengee mazingira ya namna hiyo na soma wakati wote iwe katika basi au kabla
ya kulala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni