Jumatano, 26 Oktoba 2016

NA.111 - NA.115: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.



111.  Soma kitabu kiitwacho “The Art of the Leader” kama kilivyoandikwa na William A. Cohen. Ni kitabu chenye mvuto na uhalisia.

112. Jenga hali ya kuwa na mvuto wa kipekee. Zifuatazo ni tabia kumi za kiongozi mwenye mvuto:
   Kujituma katika jambo unalolifanya.
   Muonekano kama mshindi na utendaji wa kipekee.
   Kuwa na ndoto kubwa na maono.
   Uthabiti katika kuelekea malengo.
   Kwa kila jukumu la kufanya hujiandaa na kufanya kwa bidii.
   Jijengee ustadi wa kipekee mwenyewe.
   Kujifunza toka kwa wengine na kuwa na huruma.
   Uwezo mkubwa wa kuchekesha.
   Tabia ya ujasiri inayojulikana kwa wengine.
   Kuwa mzuri wakati wa mashinikizo. (John F. Kennedy alisema hivi "the elusive half-step between middle management and true leadership is grace under pressure.")

113. Kazini onyesha uhai na upendo, cheza kwa bidii na haki.

114. Usizungumze wakati unasikiliza. Kumkatisha mwingine anapoongea ni tabia ya watu wasio na heshima. Sikiliza kama mwenye shauku kubwa ya maendeleo kwa umakini mkubwa. Utashangaa kile utakachojifunza na namna ushauri wako utakavyo hitajika na wengi.  

115. “Mtu yeyote aweza kukasirika- hiyo ni rahisi tuu; lakini kukasirika kiuhalisia, na kwa kiwango sahihi, na kwa wakati sahihi, na kwa dhumuni sahihi, na kwa namna halisi- hilo si rahisi kutokea kwa kila mtu.” - Aristotle

Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)
 

Hakuna maoni: