Jumatatu, 24 Oktoba 2016

NA.101 – NA.105: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA

101. Kitulizo cha akili ni kuridhika. Uroho na kutamani kila kitu lazima kudhibitiwe ili kuwa shwari na furaha isiyoisha. Hunabudi kuridhika na kile ulichonacho. Je una tamaa ya kuwa na vitu vyote? Mtu anaweza kuridhika ikiwa atakuwa na tabia ya uvumilivu, kujipa moyo na kujishughulisha kwa bidii katika maisha yake yote kwa shauku ya uaminifu.
102. Jiongezee rafiki au jamaa mpya kila siku. Tunza orodha yao na mawasiliano yao. Utajiri katika mahusiano ni kinasaba cha utajiri, thawabu ya maisha yako.
103. Kumbuka msemo wa wahenga wa kihindi usemao, “ukiishinda akili yako, umeushinda ulimwengu”. 104. Chagua kujibidiisha kudumu katika furaha kuliko kujipagawisha na mrundikano wa mambo kichwani kwako. Bidii katika maisha inaendelezwa na kwaumakini inalelewa na kushughulishwa kwa uangalifu.
105. Tofauti na mawazo ya wengi, msongo siyo kitu kibaya. Msongo hutusaidia kufanya vizuri zaidi na pia hutusaidia mlundikano wa sumu mwilini kutoka kwa wepesi. Ubaya ni kuwa na msongo uliopita kiasi. Au wa mara kwa mara bila kurejea hali ya kawaida. Ni lazima kuweka mizania sawa kati ya msongo na wakati wa kupumzika ili kuwa na afya iliyo njema. Viongozi wengi tulionao utaona walianza kwa kuwa na shughuli nyingi na majukumu yasiyopimika kiofisi au vinginevyo. Lakini utaona wana afya njema kwakuwa waliweka mizania ya muda wa mapumziko na kazi ndio maana utawaona ni wenye afya njema.Kwa mfano;- Raisi Kennedy alikuwa na kawaida ya kulala kidogo sana katika ofisi yake. Winston Churchhill kadhalika alikuwa na tabia hiyo hiyo akiwa na utaratibu wa kulala saa moja ofisini kwake mchana ili kuhakikisha anabaki katika hali nzuri. Si tu kwamba unapaswa kuwa huru kimwili ili kuifanya afya yako iwe njema lakini kila mmoja lazima ajenge tabia hii ya kuwa shwari kiakili. Wengine hudhani juhudi katika mazoezi, lishe bora na shughuli za kufurahisha ni suluhu ya magonjwa yote. Hivyo ni sehemu tuu lakini lazima viende sambamba na kuwa na mtizamo chanya na mawazo yaliyotulia kwa furaha ya kweli na ya kudumu.

Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya  georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: