Kama
tulivyoona katika somo lililopita njia ya mafanikio kwamba mafanikio ni safari
ambayo haina mwisho au mwisho wa safari ya mafanikio yako ni kifo. Tuliona kuwa
kila mtu Mungu amefanya uwekezaji ndani mwako tangu siku ile ulipozaliwa na
hazina tuliyowekezwa ndani mwetu ni sawasawa kabisa. Kwahiyo unao uamuzi
mwenyewe kutaka uwe masikini au kutaka uwe tajiri. Maana kila mmoja wetu
amepewa kuchagua na hakuna atakaye kusurutisha uende upande Fulani
Kumbukumbu la Torati 30:19 “ nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo,
kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana basi chagua uzima
ili uwe hai wewe na uzao wako”. Hapo ndipo kwenye tatizo la msingi wetu
wa mafanikio maana ukichukia umasikini basi umechagua utajiri kadhalika kinyume
chake. Tuendelee basi leo kuona katika barabara ya mafanikio tuweje au ni vitu
gani tuchukue katika safari yetu ya mafanikio.
- Bei inayotakiwa ni lazima iwe sawa na thamani ya kitu unachokihitaji, ni lazima matokeo ya kile unachokifanya yakupe msisimko wa kupata kitu hicho na ndivyo utakavyojikana kwa mambo yote kwakuwa kuna hamasa ndani mwako juu ya shauku uliyonayo kwa matokeo unayo yatarajia.
- Mafanikio ya mtu/watu yanaonesha utofauti kwamba huyu mwanzo alikuwa vile na sasa yupo hivi. Ili uweze kufanikiwa hunabudi kuchimbua misingi yako ya maisha katika kukufanya ufanikiwe.Kamwe usikubali kuwa vilevile kila siku, jioneshe kuwa kuna tofauti na kama tofauti haionekani basi rejea misingi yako na kuona ni wapi umekwama.
- Kujitathimini wewe mwenyewe na kuzidi kufanya marekebisho katika kuboresha mikakati yako ni jambo la msingi sana katika safari ya mafanikio. Kamwe usingojee mtu mwingine akutathimini kumbuka ni wewe binafsi uliyeamua kwamba unataka uelekee wapi, hivyo jitathimini mwenyewe na chukua hatua.
Karibu
sana tuendelee kipindi kijacho.
MtegaGFA,
“www.ujasiriamaliafya.blogspot.com”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni