Jumanne, 31 Januari 2017

Faida ya mahindi ya kuchoma!

Katika Hekta moja tunatarajia vipimo vya upandaji ni 80cms kwa 50cms na kila shimo mbegu mbili katika Hekta moja. Hivyo basi ndani ya Hekta moja utakuwa na mashina 50,000 na ikiwa umepanda kitaalamu na unahitaji uuze mahindi ya kuchoma, basi fahamu maeneo mengi mhindi mmoja wa kuchemsha au kuchomwa ni shilingi 500 ya Ki Tanzania. Kwa msingi huo mashina 50,000 zidisha mara shilingi 500 utapata shilingi 25,000,000 pesa hizi unazipata ndani ya miezi mitatu kwa gharama isiyofikia shilingi 600,000. Unaona sasa kumbe kilimo cha mahindi kinaweza pia kukutoa kimaisha mpendwa msomaji. Nikutakie siku njema!!!

Hakuna maoni: