Mafanikio ni nini?
Mafanikio ni tendo au hali ya kupata kitu ambacho ulikuwa ukikitamani sana na kuhangaika kukitafuta kwa shauku ili kiwe sehemu ya maisha yako. Na baada ya kukipata kitu hicho kinakupa furaha au burudani katika moyo wako.
Ni hatua anayofikia mwanadamu ya kuwa juu ya wengine kiasi cha kuwafanya wapende au kutamani kusikia kutoka kwake au wawe na jambo la kujifunza toka kwake.
Vitu gani vinaweza kukufanya ufanikiwe?
Kwakuwa katika safari ya mafanikio siyo rahisi sana, ndiyo maana si kila mtu amefanikiwa, kumbe utaona vipo vitu ambavyo mtu huyu akiwa navyo ndani mwake basi mafanikio yatakuwa dhahiri katika maisha yake!
Ujasiri: Unapaswa kuwa jasiri usiyekata tamaa kwa kuangalia mazingira yaliyo kuzunguka na vikwazo vyake hadi ufikie lengo lako. Ujasiri unahitajika katika maeneo mbalimbali kama ya kibiashara, kiuchumi na kisiasa, bila ujasiri huwezi kufikia malengo unayoyatamani katika maeneo hayo.
Hatua kuyaendea mafanikio;-
Ubunifu: uchunguzi na ukusanyaji taarifa zihusuzo jambo unalotaka kulifanya.
Kuatamia wazo: wazo ukishalipata ni lazima uliatamie kwani inawezekana wazo ni jipya kabisa hivyo lipe muda huku ukitafakari litatotolewa tuu.
Uzoefu: kadiri unavyokaa na wazo hilo na kuruhusu akili ilifanyie kazi kwa muda unajipa uzoefu mwenyewe wa kulifanyia kazi wazo lako.
Kutathimini na kutekeleza: baada ya kupitia hatua hizo unapaswa kufanyia tathimini taarifa ulizonazo juu ya wazo lako na mara moja kuanza utekelezaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni