Mpendwa rafiki yangu na mfuatiliaji wa Makala za kurasa zetu za "Ujasiriamaliafya" kwanza napenda kukushukuru kipekee kwa jinsi ulivyokuwa bega kwa bega kufuatilia makala zetu pamoja na hatua mbalimbali katika kutendea kazi. Hakika hatua uliyokwisha kuchukua ni kubwa sana kwani ndivyo safari ya kuwa mtu mashuhuri au tajiri katika jamii ndivyo inavyo anza. Kubwa ninalopenda kukushirikisha siku hizi za sherehe za mwisho wa mwaka ni kwamba, ili tuweze kuutendea ipasavyo mwaka 2016 hatuna budi kufanya na kufahamu yafuatayo:-
1.Fahamu kwamba majira ya sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi na mwaka yamekuwapo kwasababu maalum.
2.Majira haya kamwe hayafanani ndio maana kila yanapokuja tunaita majira mapya.
3.Weka Mipango yako ya nini unakusudia kutekeleza Januari hadi Desemba mwakani 2017.
4.Weka mikakati sasa ya jinsi ya kuyafikia malengo yako.
5.Hakikisha malengo hayo yanatekelezeka.
6.Kumbuka kumshirikisha Mungu ratiba hiyo na mikakati yako faraghani yaani katika maombi.
7.Hakika 2017 ni mwaka mpya na utasimulia mwishoni kwamba maisha yamebadilika kabisa.
Nikutakie maandalizi mema!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni