Jumamosi, 15 Oktoba 2016
NA.77 - NA.80: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.
77. Kamwe usijadili shughuli zako binafsi za maendeleo na mtu mwingine! Mikakati ya kutanua maendeleo yako na yale unayojitia moyo katika nafsi yako ni vyako mwenyewe. Ukiwashirikisha wengine wanaweza wasijue jinsi ulivyojipanga na ramani yako na hivyo wanaweza kukukwamisha, na zaidi wapo wengine ukiwashirikisha watakuvunja moyo ili uache na wao wanachukua ramani hiyo na kuifanyia kazi. Ifanye mikakati yako ya kimaendeleo kuwa ni yako tuu na kama kuwashirikisha wengine utawashirikisha baada ya kufanikiwa ukiwaongoza waende kama ulivyoendea ramani yako.
78. Panga muda wa mapumziko ndani ya wiki na kusiwe na chochote kitakachoibadili ratiba yako, hapa unatakiwa kuwa mkatili katika kuitunza ratiba yako. Huu ni muda wa kuijenga afya yako ambayo ndio uwekezaji namba moja juu ya yote unayotaka kuyafikia. Kama ilivyo vigumu kubadili ratiba ya kuonana na Raisi au mtu yeyote mashuhuri hapa napo panahitaji nidhamu hiyo na kuzidi. Ni lazima kujiwekea muda wa kupumzika ambapo utatafakari utendaji wako na kujipanga upya pale ulipokwama na hii itakuongezea ari kubwa ya kufanya vizuri zaidi.
79. Asilimia 83 ya hisia zetu huja kutokana na vitu tunavyoviona kwa macho yetu. Ili utafakari kikamilifu juu ya jambo fulani, funga macho ili kuondoa muvutano na vitu vingine utakavyo viona katika kutafakari kwako.
80. Uwe mtawala wa ridhaa au hiari yako bali uwe mtumwa wa dhamiri yako. Dhamiri ni kitu kile unachokisikia ndani mwako. Unaweza kuwa na jambo gumu linalohitaji kufanyika sasa kwa utashi wako. Hapo uwanja wa dhamiri ndipo hujitokeza na kukwambia fanya hivi na acha hili. Sauti hiyo ukiweza kuisikiliza kwa umakini na ukaitendea kazi mara moja mafanikio ni lazima!
Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni