Ijumaa, 14 Oktoba 2016

NA.73 - NA.76: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.


73. Kubeza mazoea ni kanuni nzuri sana! Nyota za anga zinaendelea kuwa mbali kabisa na dunia. Unapaswa kuwa mbali na yote bila kuathiri mahusiano na wengine. Hali inayoashiria wema au ubaya wa mtu hupotea au kutoweka pale unapoona kila kitu juu ya kiongozi wako kutokana na ustadi wa pekeyake aliokuwa nao katika mamlaka yake. Mfano ‘Ronald Reagan” aliyewahi kuwa rais wa marekani alijulikana na wengi kwamba alikuwa ni kiongozi mzuri sana. Kwa umakini mkubwa alijenga tashwira kuwa ni mcheshi, na kufikiriwa kuwa alikuwa ni mwanasiasa aliyeweka mbele wakati wote maslahi ya watu wa Amerika. Jee uliwahi kumuona raisi akiwa amevua nguo zake za kawaida na kuvaa nguo za kuogelea katika bwawa lake la kuogelea? Vipi kuhusiana na nguo zake za kulalia baada ya kuwa ametoka katika kulala usingizi mzito? Kamwe raisi Reagan hakuwahi kujiweka wazi kihivyo kwani aliamini kufanya hivyo ingemshusha hadhi yake ya kiuongozi. Hivyo basi waamerika hawakuwekwa wazi kabisa katika jambo hilo. Hata hivyo katika kipindi cha raisi Bill Clinton mambo yakabadilika tunaona raisi akila chakula hadharani, akivaa kofia ya wacheza mpira wa magongo na suti yake ya kazi. Kumbe matukio hayo yanakufanya upendeke na jamii, hapa nadhani Clinton ilimfanya aonekane yupo pamoja na watu aliokuwa akiwaongoza, tofauti na nyota za anga zinazoonekana karibu chini kabisa.
74. Jifunze kuupanga muda wako. Si sahihi kusema mtu anayesimamia na kuwa muangalifu juu ya muda na kuishi kwa umakini mkubwa katika kuzingatia ratiba unakuwa ni mtu usiyeshawishika. Badala yake inakufanya kukamilisha majukumu yako kwa wakati na kuwa na muda mwingi wa kufanya majukumu mengine au kupumzika. Vilevile ni kujiwekea nidhamu binafsi ya kuujali muda wako na kuacha kupoteza muda kwa vitu ambavyo hukupangilia japo ni vizuri lakini si vya muhimu (mf. Matumizi ya simu) na tafakari juu ya shughuli zile ambazo ni kwa hakika zina umuhimu katika malengo ya maishani mwako. Shughuli hizo ni pamoja na kujikumbusha mambo mabalimbali na kutafakari juu ya malengo yako, matumizi mazuri ya muda yanakujengea imani na heshima katika majukumu yako, muda wa mazoezi ya kuujenga mwili, muda wa kusoma na kutafakari pamoja na muda wa kuwahudumia wengine.
75. Hakikisha unajiweka vizuri kujua matukio au mambo yanayoendelea, matoleo mapya ya vitabu na mambo mengine yanayoigusa jamii kwa ujumla. Wengi wa waliofanikiwa sana, husoma makala tano hadi sita kwa siku moja. Hupaswi kusoma kila kitu katika makala hiyo. Fahamu kitu gani unakusudia kukisoma kwa umakini, nini utakipitia tuu na kipi ambacho utapaswa kukirudia tena na tena (watu waliofanikiwa huchuja na kulipima kila gazeti au makala anayoisoma, kuweka notisi ya yale yakumfaa na kuyakusanya kwa pamoja kwa lengo la kuyarudia tena na tena). Ufahamu wa jambo ni nguvu! Iwe ni mjasiriamali, kiongozi wa taasisi, au yeyote anayeongoza familia, Unaweza kabisa kubadili maisha ya wale unaowaongoza au waliochini yako kwa wazo moja tuu. Waulize akina Gates, Edison na Bell watu maarufu hawa jinsi walivyoweza kuibadili dunia.
76. Katika kumchagua mbia au mwenzi wa maisha, kumbuka kwamba huu ni uamuzi muhimu sana katika maisha yako yote. Mahusiano ya wanandoa yanakupa 90% ya msaada kwako, furaha na kukidhi kwako, kumbe sasa chagua mwenzi wako kwa hekima na si kwa tamaa. Fikiria ubora kama upendo, hisia za ucheshi, uelewa, maadili, ukomavu, tabia, kushikamana, sifa zingine zisizoelezeka kama za kikemikali. Kama vyote hivyo vipo basi mahusiano yako yatadumu na ninafasi nzuri ya kuyafikia mafanikio makubwa. Nenda taratibu na usiruhusu mwingine akufanye utoe maamuzi ambayo yatakufanya usiyafurahie baadaye.
Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya georgemtega@gmail.com au Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: