Mpendwa msomaji na
rafiki yangu katika mtandao wetu wa kijamii! Salaam!
Nimeanzisha mtandao huu
kwa nia ya kushirikishana mambo mbalimbali yahusuyo Ujasiriamali na Afya kwani
baada ya kupitia makala mbalimbali za Waandishi mbalimbali maarufu duniani na
wana-falsafa mbali mbali nimegundua hakuna mwanadamu yeyote ambaye amezaliwa
ili awe masikini licha ya wengi kudhani kuwa umasikini ni sehemu ya jamii fulani
au familia fulani. Blog yangu inaitwa “ujasiriamaliafya” hapa yameunganishwa
maneno mawili ujasiriamali na afya. Hii ni kwasababu mjasiliamali yeyote ili
kufikia ndoto za mafanikio yake hana budi kuwa na afya njema. Hivyo basi mambo
ambayo tutashirikishana hapa ni yale yahusuyo mafanikio na afya zetu.
Kubwa la kufahamu hapa
na kulikumbuka ni kwamba “akili yako mwenyewe ndiyo yaweza kukufanya uwe
masikini au tajiri” hii ni kwasababu mambo yote yanaanzia kwenye akili. Jinsi
unavyojiona na jinsi unavyojisikia na kujitambua ndiyo maisha yako yatakavyokuwa.
Endelea kufuatilia
mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni